top of page
  • Writer's pictureSilent Poster

WHO chanjo dhidi ya Coronavirusi

hirika la Afya Duniani,WHO limezidua rasmi  chanjo  ya majaribio dhidi ya COVID – 19 .

Hatua hii ni kufuatia ongezeko ya maambukizi na vifo duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amewapongeza watafiti kote duniani ambao wamejumuika pamoja ili kutaathimini majaribio haya.



Dkt Ghebreyesus akisema hatua hii ni  mafanikio makubwa na kuwa kwa sasa wataalamu wa afya yanafanywa kila juhudi kuhakikisha kuwa tiba yeyote ambayo itasaidia kuokoa maisha imepatikana

Amesema hata kama kuwa uwezekano wa kutofata mafanisi kutokana na majaribio madogomadogo na njia mbalimbali,tiba ya haraka inahitajika na kuna uhakika itapatikana .


Zaidi ya hayo,Dkt. Ghebreyesus,ameongeza kuwa WHO na washirika wake wanaandaa utafiti katika nchi mbalimbali ambapo baadhi ya dawa hizi hazijafanyiwa majaribio zitalinganishwa .

Amesema utafiti huo mkubwa unaandaliwa kwa minajili ya kukusanya takwimu zinazohitajika ili kubainisha ni matibabu yapi yanafayakazi zaidi.

Licha ya hayo, nchi kadhaa tayari zimethibitisha kwamba zitashiriki utafiti huo wa  Mshikamano wa majaribio.

Nchi hizo ni kama vile, Argentina, Bahrain, Canada, Ufaransa, Iran, Norway, Afrika Kusini, Hispania, Uswisi na Thailand.

Kuna matumaini kuwa nchi zingine ulimwenguni zitajiunga ili kuhakikisha jawabu au tiba ya COVID -19 imepatikana.Jambo ambalo WHO imelichangamkiakwani linatia moyo


Dkt. Tedros anasema kuwa hatua za mshikamano dhidi ya COVID-19 kumepelekea mchango wa zaidi ya dola milioni 43 kutoka kwa watu zaidi ya 173,000 na mashirika hisani siku chache tu tangu ulipozinduliwa.

FIFA ni baadhi ya mashirika ambayo yamechangia mfuko huu kwa kutoa dola milioni 10.

Utafiti huo umepewa jina la “Majaribio ya mshikamano”.

Amesisitiza kwamba virusi hivi ni tishio kubwa lakini kwa pamoja litakabiliwa.Isitoshe, WHO imesema kuna hofu jinsi Bara la Afrika linavyochukulia janga hili.

Hapo awali takwimu zilionyesha maambukizi yalikuwa kiwango za chini barani Afrika lakini mambo yamebadilika kwa kasi huku idadi ya maambykizi ya kuongezeka.

Ametaka serikali za Afrika kuchukua janga hili kwa dharula ili kulikabili.

Taharuki imetanda nchi DRC baada ya visa 600 kuripotiwa.

serikali ya Congo imejitahidi kukabiliana na hali hii

0 views0 comments

Recent Posts

See All
bottom of page