top of page
  • Writer's pictureSilent Poster

Askofu Getrude Rwakatare

MAMA GETRUDE RWAKATARE AFARIKI DUNIA


Kifo cha Askofu Rwakatare kimepokelewa na waliomfahamu kwa huzuni na majonzi.

Mawanawe Muta Rwakatare,alitoa taarifa ya kifo cha mamake.Anasema Askofu alikuwa na matatizo ya moyo na alifariki hospitalini ambapo alipelekwa baada ya kuugua ghafla.



Alikuwa ni mtumishi wa Mungu,Mbunge maalum na mwanabiashara mashuhuri nchini Tanzania

Askofu Daktari mama Rwakata alikuwa na maneno na sauti nyororo ya kumtoa nyoka pangoni.


Mahubiri yake yalikuwa na warsia na alinena kwa ukakamavu wa mama shujaa.


Nakumbuka wakati mmoja nilipozuru Dar es salam ,marafiki wangu wakanikaribisha kutembelea kanisa la Mlima wa moto pale mikocheni B.

Nilipoketi na kusikiriza mafunzo/mahubiri yake mama Rwakatare nilijihisi kama nimezaliwa tena kiroho, tangu wakati huo nilipenda kusikiliza mahubiri yake kwenye televisioni .


Alikuwa kwenye mstari wa mbele kwenye maswala ya usawa wa jinsia hasa maswala na kina mama na maendeleo.

Wakati mmoja alisimulia historia ya maisha yake kimasomo,ndoa na jinsi alijitahidi kupata mali kama mwanamke mwenye juhudhi pasipo kumtegemea mumewe.


Mchungaji Rwaktare alizaliwa Kilombelo ,huko morogoro, akasomea Korogwe na baadaye akaenda nchini Kenya kwa masomo ya Chuo kikuu katika Chuo Kikuu Cha Nairobi.


Alikuwa ni msomi aliyekuwa na hamu ya kuona kila mtanzania amepata elimu ya hali ya juu.


Hii ilipelekea yeye kuanzisha shule za St Mary ambapo watanzania wengi walio kwenye nyaja mbalimbali nchini wamepitia.


Aliwarai akina mama kutia bidi katika shughuli zao za kila siku kwani bila bidii ,hakina faida.


Alikashfu uvivu.chimbuko la umaskini alisema ni uvivu.Alisema ni muhimu watu waajibike,watumike ,wajiajiri hasa vijana na akina mama.


Fahari na heshima ya mwanaume alisema ni kazi


Aliwatia moyo walokata tamaa maishani kwa kuwalisha chakula cha kiroho na kwa kutoa mawaidha .


Mola ailaze roho yake palipo watakatifu wake …Amina

5 views0 comments

Recent Posts

See All
bottom of page