top of page
  • Writer's pictureSilent Poster

Donald Trump asitisha WHO msaada

Updated: May 1, 2020

Shirika la Afya Duniani, (WHO) limetangaza ongezeka ya maambukizi na vifo vya virusi vya Corona.


Takwimu zinaonyesha ongezeko ya maambukizi hadi milioni 2 kufikia sasa,huku vifo vikiwa elfu 131.


Marekani na mataifa ya Uropa yanaongoza katika vifo na maambukizi duniani.


Marekani imerekodi vifo elfu 28,326 na maambukizi elfu 637.

Ikifuatiwa na Italiano na vifo 21,645,Uhispania nayo ni ya tatu na maafa ya kiwango cha 18,579.


Ufaransa inachukua nafasi ya nne na vifo Zaidi ya elfu 17 huku Uingereza ikiwa ya tano na vifo elfu 12.


Tarifaa hii inatolewa siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusitisha mswada wa fedha kwa Shirika la Afya Duniani kwa kile alichokitaja kama kutoa taarifa za kupotosha kuhusu maambukizi ya Corona na pia kuelekeza juhudi zake nyingi Uchina katika shughuli za kukabiliana na ugonjwa wa Corona.





Hata hivyo, hatua ya Trump imeshutumiwa na viongozi wa mataifa mbalimbali duniani kwani haukuwa wakati mwafaka wa kuchukua hatua kama hiyo; hasa wakati dunia inapotafuta shuluhu ya dharula kukomesha maambukizi ya COVID 19.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom, amesema kuwa nimatumaini yake Marekani ataendelea kuwa mshirika wa karibu wa shirika hilo kama ambavyo amekuwa kwa muda mrefu.


Mataifa tajiri duniani G20 yametangaza kuahirisha malipo ya madeni yake kwa mataifa yaliyo na mikopo kwa muda wa mwaka mmoja.


Kufikia sasa, mataifa mengi yameanza kurejerea katika hali ya kawaida huku baadhi ya mengine yakichukua tahadhari kuhakikisha hali imekabiliwa.


Nchi ya Denmark na Ugeremani masomo yamerejea huku mataifa ya utaliano na uhispania wakirejea kazi kwa baadhi ya kampuni.


Nchini Kenya hatua zimechukuliwa na serikali kuhakikisha kila mtu anajikinga ipasavyo ilikuepuka maambukizi.


Hatua kali zimewekwa kwa wale watakao kiuka maagizo ya serikali.


Pia usafiri wa sehemu za majimbo zimekatizwa na wanaoishi miji ilioko karibu na jiji la Nairobi wanapaswa kuwa nyumbani ifikapo saa moja kamili.


Idadi ya maambukizi Kenya imefika 225 huku vifo vikiwa kumi hadi sasa.


Jimbo la Nairobi linaongoza katika maambukizi ya watu 163,Mombasa ikifuata na watu 36 Kilifi ikiwa na watu kumi huku mandera ikiwa na watu sita.

1 view0 comments

Recent Posts

See All
bottom of page