top of page
  • Writer's pictureSilent Poster

Silas Njiru-Askofy

Updated: May 1, 2020

Askofu mstaafu Silas Njiru Afariki dunia

Virusi vya Corona vimepokonya kanisa katoliki na Kenya kwa jumla Askofu Mstaafu wa Jimbo la Meru,Silas Njiru .


Askofu Njiru alifariki mapema Jumanne nchini Italia baada ya kuambukizwa Covid-19.


Askofu wa Meru Salesius Mugambi ambaye alichukua hatamu za uongozi wa jimbo hilo baada ya kustaafu kwa marehemu, alisema Askofu huyo mstaafu alikuwa anapokea matibabu katika Hospitali ya Rivoli ambapo alikuwa amelazwa kwa siku tatu.

Hapo awali Asofu wa jimbo la Embu kupitia ujumbe kwenye mtando, aliomba wakristo kumuombea Marehemu kwani alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi .

Alikuwa miongoni mwa mapadre watatu walioambukizwa virusi vya Corona kwenye makao yao.

Marehemu alikuwa akikaa katika nyumba ya Mtakatifu Joseph Allamano huko Alpignano, Turin, Italia tangu kustaafu kwake. Alizaliwa Mwezi 1928 katika kijiji cha Kevote, Kaunti ya Embu.

Alihudhumu katika jimbo la Meru kwa muda mrefu zaidi,pia amekuwa Padre kwa miaka zaidi  ya sitini.

Mola ailaze roho pema peopni.

  • Ugonjwa wa Corona na walio kwenye hatari

  • Watu wenye umri wa miaka sitini na zaidi

  • Walio na ugonjwa wa kisukari

  • Ugonjwa wa moyo baadhi ya maradhi mengine.


Pamoja tuangamishe Corona

2 views0 comments

Recent Posts

See All
bottom of page