top of page
  • Writer's pictureSilent Poster

kifua kikuu-WHO

Kifua kikuu --mikakati yabuniwa


Dunia imeadhimisha siku ya kifua kikuu,huku idadi ya maambuziki ikizidi kuongezeka.


Hali hii imepelekea wataalamu wa afya duniani kutafuta mikakati itakayo badili hali ili kupunguza idadi ya wagonjwa na walioko kwenye hatari ya maambukizi.


Takwimu zinaonyesha kuwa robo ya watu duniani wana backeria ya kifua kifuu mwilini na wako hatarini ya maambukizi,hasa wale walio na kinga dhaifu.


Kufuatia haya,Shirika la Afya Duniani,WHO limetoa mapendekezo, kuongezwa kiwango cha matibabu ya kuzuia Kifua kikuu kati ya idadi ya watu walio katika hatari kubwa.


Mapendekezo hayo ni kama vile:kuboresha ubunifu kuzuia hali ya wagonjwa wa kifua kikuu, watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi na pia wanaoishi katika mazingira yaliyojaa.


WHO inapendekeza kwamba ama majaribio ya tuberculin au interferon-gamma (IGRA) itumiwe kupima ugonjwa wa Kifua kikuu.


Upimaji wa maambukizo ya Kifua Kikuu,ingawa hauhitajiki kabla ya kuanza tiba ya kinga kwa watu wanaoishi na VVU, na watoto chini ya miaka 5.


Pia ,WHO inapendekeza mbinu fupi, jinsi ya kutumia dawa kukabili TB kwa kupunguza muda wa awali wa miezi 6 .


Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaoongoza kwa maabukizi,mllioni 10 na vifo vya takribani watu million 1.5 duniani mwaka wa 2018.


Juhudi hizi zinafanywa wakati dunia ikikabiliana na jinamizi la Virusi vya Corona huku Mkuu wa WHO Tedro Ghebreyesus akissitiza umuhimu wa kuendele na juhudi za kukabiliana na magonjwa haya yakuambukiza,ili kuokoa maisha.


Ingawa maendeleo yamepatikana kwenye malengo yaliowekwa kupunguza makali ya TB juhudi za nchi wanachama zahitajika zaidi ilikuafikia malengo ya kukomesha Tb ifikiapo mwaka wa 2030.


Kenya yajizatiti kuhakikisha wanaougua Tb wanapokea matibabu na pia lishe bora ili kuimalisha afya na idadi ya maambukizi.

Hata hiyo juhudi zaidi hasa mashinani zinahitajika.juhudi za kuelimisha umma na namna ya kupata matibabu iendelezwe kwa kina.


Mwaka jana Wizara ya Afya kenya ilizidua mwongozo na malengo yakupunguza maambukizi ya watu 597,000 ifikapo mwaka wa 2023



 








3 views0 comments

Recent Posts

See All
bottom of page