top of page
  • Writer's pictureSilent Poster

Dr Catherine Hamlin afariki

Daktari wa Afya ya akina mama ,Dkt Catherine Hamlin Amefariki Dunia huko Ethiopia akiwa na umri wa miaka 96.

Dkt Hamlin ni mzaliwa wa Australia na alikuja Afrika katika shughuli za kazi ya utaalamu wa afya ya wanawake. Alijitolea kwa moyo wa dhati  kuwasidia akina mama hususan nchini Ethiopia kuwanusuru kutoka kwa ugojnwa wa fistula ambao humwacha mwanamke na fedheha. Dkt  Hamlin,alikuwa mkarimu ,mwenye upendo na huruma aliye jitolea kuhakikisha mwanamke amepata matibabu yafaayo anapopatwa na hali kushindwa kudhibiti mkojo baada ya kujifungua. Alipowasiri nchini Ehiopia hakukuwa na hospitali iliyowatibu wagonjwa wa fistula ya akina mama lakini alifanya juu chini kuhakikisha namna ya kurejesha heshima na matumaini kwa  akina mama imepatikana. Pamoja na mumewe walifanya ubunifu wa kutafuta namna tofauti za kufanya upasuaji wa wanawake waliona fistula ,ubunifu ambao unatumiwa na wataalamu wa afya ya kina mama hadi sasa. Fistula ni jinamizi linalowaghubika akina mama kote duniani,lakini juhudi zake za kuwanusuru kutoka utumwa wa ugonjwa huu zilifua dafu. Marehemu atakumbukwa kwa uanzilishi wa hospitali ya Fistula, Addis Ababa kwa ushirikiano na mumewe mwaka wa 1974. Hata baada ya kuachwa mjane na mumewe aliyefariki mwaka wa 1993,dkt Catherine hakukomesha juhudi zake hapo. Alijikasa kisabuni mpaka jihudi zake zikatabuliwa kote duniani. Alitunukiwa zawadi nchini Ethiopia na pia nje ya nchi. Fistula ni ugonjwa ambao husababisha shimo kubwa kati ya njia ya uzazi na njia ya mkojo unatokana na mama kuwa na uchungu wa kujifungua kwa muda mrefu bila kushughulikiwa kimatibabu. Kwa mujibu wa Shirika la Ulimwengu la idadi ya watu, mara nyingi ugonjwa huu huwapata wanawake na wasichana kutoka nchi zilizobaki nyuma kimaendeleo na waotoka  jamii maskini kabisa. Wanaopata fistula mara kwa mara wanakubwa na unyanyapaa mkubwa kwa jamii. Licha ya kutaka kutafuta matibabu,wao kukosa uwezo wakupata hela ili kwenda hospitalini na kuishi na hali ya kudharauliwa na pia kutengwa na jamii. Ni haki ya kila mtu kupokea matibabu ,anapopata hali hii. Pia ni jukuma la mama na wasichana kuhakikisha wanafuata maagizo ya wauguzi wanapo kuwa na uja uzito ili kuepuka kuwa madhara wakati wa kujifungua. Isitoshe,tatizo la fistula linaweza kukomeshwa endapo wasichana wa umri mdogo wataepuka kupata mimba za mapema ,mila potovu za ukeketaji na pia kupata huduma za afya mapema wanapopata uja uzito. Mwaka wa 2018 takwimu zinaonyesha kuwa wanawake millioni 2 waliadhiriwa na Fistula katika Bara la Afrika. Dkt Catherine alitajwa kama mama aliyekuwa na wasichana 35,000 na wakfu wake alifanya upasuaji wa akina mama na wasichana 60,000. Mkurugenzi mkuu wa shirika la Afya Duniani,,WHO Dkt Tedro Ghebreyesus ambaye pia alimfahamu Dkt Catherine wakati akitumika kama waziri wa Afya nchini Ethiopia  alimtaja marehemu kama mtu Mkarimu ,mwenye utu na akasema juhudi zake kitaendelezwa na waliobaki. Mwanamke Ngangari,Marehemu Catherine Mola ailaze roho yake pema peponi..

3 views0 comments

Recent Posts

See All
bottom of page