top of page
  • Writer's pictureSilent Poster

Ken Walibora amefariki

Updated: May 1, 2020

Ken Walibora ameaga dunia.


Mwandishi wa Riwaya ya Siku Njema na wanahabari mtajika Ken walibora amefariki .



Inadaiwa mwanahabari/mtangazaji alipatikana katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali kuu ya Kenyatta.


Marehemu aligongwa na gari katika barabara ya Ladhies na gari la usafiri wa umma siku ya Ijumaa.


Hakika Walibora alitukuza kiswahili....

Walibora amechangia katika maendeleo ya Lugha hasa ya Kiswahili kwa kuandika vitabu kama vile Siku Njema na Kidagaa kimemwozea,Ndoto Ya Amerika ,nasikia sauti ya mama,Ndoto ya Almasi ,Kufa Kusikana na vingine vya kimombo. Zaidi ya hayo,Walibora alifanya kazi na kampuni ya Utangazaji ya Nation kama mhariri wa kitengo cha kiswahili. Baadaye alisafiri hadi Marekani alipokuwa mhadhiri wa lugha ya afrika.


Kifo chake kimetokea baadaya waandishi wawili wa kampuni ya Nation kugongwa na gari katikati mwa jiji la Nairobi.


Mola amlaze pema peponi ustadh,malenga Walibora


5 views0 comments

Recent Posts

See All
bottom of page